NA;RAPHAEL MALEKELA
TUVITA
(TUNAWEZA VIJANA TANZANIA)ni taasisi isiyo ya
kiserikali,imeanzishwa kwa lengo la kuwasaidia vijana kwa ujumla wake
kuondokana na maisha ya uharifu,kuishi kinyume na taratibu za mila na desturi
za mtanzania,kuondokana na tabia za uvivu wa kufanya kazi zenye kuleta
maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla.
Taasisi hii yenye makao makuu yake jijini Dar es
Salaam,itakuwa ikitoa elimu hiyo kwa vijana nchi nzima katika maeneo mbalimbali
ya kijamii kama vile mashuleni,vyuoni,na kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya
watu nayo ni masokoni na kwenye viwanja vyamichezo na kwenye taasisi mbalimbali
mijini na vijijini.
Elimu hiyo itakuwa ikitolewa kwa njia ya mafundisho
kwa kutoa mada mbalimbali,kwanjia ya sanaa kama
uimbaji,njonjera,mashairi,maigizo na michezo mbalimbali yenye kufikisha ujumbe
salama kwa vijana.Pia tuvita itashirikiana na wizara mbalimbali katika kutoa
elimu kwa vijana,wizara hizo kama wizara ya mambo ya ndani ya nchi,wizara ya
kazi ajira na maendeleo ya jamii,wizara ya habari michezo na utamaduni,na taasisi ya kupambana ya
rushwa,na kitengo cha kupambana madawa ya kulevya,hata hivyo taasisis hii hata
funga kushirikiana na wizara zingine za serikali na taasisi zake zote.
Hii inatokana na kuwepo kwa wimbi kubwa la
mmomonyoko wa maadili na uharifu katika jamii jambo ambalo ni tishio kwa
nguvukazi na usalama wa taifa letu.matukio mengi ya kiuharifu yanaporipotiwa
wahusika wakubwa ni vijana tena wenye umri mdogo,ambapo hawa wakipewa elimu ya
kujitambua na kuona umuhimu wao katika familia,jamii hadi taifa vijana hawa
watakuwa chachu kubwa katika kuleta maendeleo,
TUVITA kwa kushirikiana na serikali itakuwa
inatafuta fursa mbalimbali za kiajira katika mashirika na makampuni
mbalimbali,lakini kubwa zaidi kuhamasisha vijana katika eneo la kujiajiri
katika maeneo mbalimbali kama ufundi,kilimo,ufugaji wa wanyama na jamii ya
ndege kama kuku na bata kwa vijana wakiwa katika vikundi vidogovigo vitakavyo
tambuliwa kisheria vikiwa chini ya ulezi wa tuvita.
TUVITA hivi sasa ipo katika taratibu wa usajili kwa
mujibu wa sheria na taratibu za nchi zilizopo,na kuomba ushiriano kutoka kwa
wananchi katika kuwalea vijana katika maisha yenye maadiri ya uaminifu na
utiifu katika kufanyakazi.
TUVITA inasema huu si wakati wa klaumiana juu ya
mmomonyoko wa maadiri kwa vijana ndani ya taifa letu,kwakushirikiana na
kushikamana pamoja na kuwa na kauli moja tutawakomboa vijana na jamii na taifa
litakuwa lenye nguvu kiulinzi na uchumi.
No comments:
Post a Comment