Thursday, May 28, 2015

TUVITA KUWA MKOMBOZI WA VIJANA TANZANIA



NA;RAPHAEL MALEKELA

TUVITA (TUNAWEZA VIJANA TANZANIA)ni taasisi isiyo ya kiserikali,imeanzishwa kwa lengo la kuwasaidia vijana kwa ujumla wake kuondokana na maisha ya uharifu,kuishi kinyume na taratibu za mila na desturi za mtanzania,kuondokana na tabia za uvivu wa kufanya kazi zenye kuleta maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla.

Taasisi hii yenye makao makuu yake jijini Dar es Salaam,itakuwa ikitoa elimu hiyo kwa vijana nchi nzima katika maeneo mbalimbali ya kijamii kama vile mashuleni,vyuoni,na kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya watu nayo ni masokoni na kwenye viwanja vyamichezo na kwenye taasisi mbalimbali mijini na vijijini.

Elimu hiyo itakuwa ikitolewa kwa njia ya mafundisho kwa kutoa mada mbalimbali,kwanjia ya sanaa kama uimbaji,njonjera,mashairi,maigizo na michezo mbalimbali yenye kufikisha ujumbe salama kwa vijana.Pia tuvita itashirikiana na wizara mbalimbali katika kutoa elimu kwa vijana,wizara hizo kama wizara ya mambo ya ndani ya nchi,wizara ya kazi ajira na maendeleo ya jamii,wizara ya habari michezo  na utamaduni,na taasisi ya kupambana ya rushwa,na kitengo cha kupambana madawa ya kulevya,hata hivyo taasisis hii hata funga kushirikiana na wizara zingine za serikali na taasisi zake zote.

Hii inatokana na kuwepo kwa wimbi kubwa la mmomonyoko wa maadili na uharifu katika jamii jambo ambalo ni tishio kwa nguvukazi na usalama wa taifa letu.matukio mengi ya kiuharifu yanaporipotiwa wahusika wakubwa ni vijana tena wenye umri mdogo,ambapo hawa wakipewa elimu ya kujitambua na kuona umuhimu wao katika familia,jamii hadi taifa vijana hawa watakuwa chachu kubwa katika kuleta maendeleo,

TUVITA kwa kushirikiana na serikali itakuwa inatafuta fursa mbalimbali za kiajira katika mashirika na makampuni mbalimbali,lakini kubwa zaidi kuhamasisha vijana katika eneo la kujiajiri katika maeneo mbalimbali kama ufundi,kilimo,ufugaji wa wanyama na jamii ya ndege kama kuku na bata kwa vijana wakiwa katika vikundi vidogovigo vitakavyo tambuliwa kisheria vikiwa chini ya ulezi wa tuvita.

TUVITA hivi sasa ipo katika taratibu wa usajili kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi zilizopo,na kuomba ushiriano kutoka kwa wananchi katika kuwalea vijana katika maisha yenye maadiri ya uaminifu na utiifu katika kufanyakazi.

TUVITA inasema huu si wakati wa klaumiana juu ya mmomonyoko wa maadiri kwa vijana ndani ya taifa letu,kwakushirikiana na kushikamana pamoja na kuwa na kauli moja tutawakomboa vijana na jamii na taifa litakuwa lenye nguvu kiulinzi na uchumi.  

Friday, May 22, 2015

MVUA JINSI ZILIVYO HARIBU MIUNDOMBINDU


Daraja linalowaunganisha wakazi wa Monolandege na Mombasa jimbo la Ukonga kata ya Ukonga manisipaa ya Ilala likiwa limesombwa na maji ya mvua hivi karibuni nakuta mawasiliano ya huduma za kijamii kwa wakazi hao

  Mwenyekiti wa kamati ya mindombinu (kulia) ndugu Elly Dallas Mtaa wa Mongolandege kata ya Ukonga     akiangalia ubovu wa barabara katika mtaa huo uliyo sababishwa na mvua zilozonyesha hivi karibuni.

Hivi ndivyo ilivyo kwahali ya barabara mtaa wa Mongolandege kata ya Ukonga