Monday, February 25, 2013

JAMII YATAKIWA KUACHA UKATIRI DHIDI YA WATOTO


Jamii imetakiwa kuacha vitendo vya ukatiri dhidi ya watoto,badala yake wawalee watoto hao katika malezi bora yatakayowafanya watoto wawe na furaha wakati wote.
Hivi karibuni maeneo ya ukonga mazizini katika manispaa ya Ilala,kitendo cha kikatiri dhidi ya mtoto Deo Laulent,mwenye umri wa miaka 7,anaesoma darasa la kwanza katika shule ya msingi Amani mzambarauni ukonga,yamemkuta makubwa na kumpelekea kujeruhiwa vibaya usoni na kichwa kama anavyo onekana pichani.

Kitendo hiki kimedaiwa kufanywa na mama yake mzazi bi Gradi David,mkazi wa mtaa wa mazizini ukonga,alimuazibu mtoto kwa kosa la kutokwenda kula chakula kwa mama yake mkubwa baada ya kutoka shule mchana,kwa maelezo ya mtoto huyu,anakiri kuagizwa kwenda kula kwa mama mkubwa,lakini akajikuta ameenda kucheza kwa rafiki yake aliyemaja kwa jina la Juma,kwa maelezo yake mtoto Deo,alicheza kwa rafiki yake,alikula chakula cha mchana na baadae kuoga kwa huyo rafiki yake,ambapo alishinda huko hadi jioni na kurudi nyumbani kwao.

Aliporudi nyumbani Deo alipewa sh 1000 na bibi yake[mjumbe wa shina] ambae ni mwenyenyumba alipopanga mama yake,akanunue chips ale,ambapo bibi huyo hufanya hivyo mara kwa mara,ambapo mama yake Deo anapotoka kwenye kazi yake hulipa pesa hizo,mama yake Deo ni muhudumu wa bar maeneo ya banana.

Mama yake Deo,alipokuwa anarudi toka kazini kwake majira ya usiku alipia kwa muuza chips ambapo mtoto wake alinunua,akaambiwa mtoto wake amekula chips za tsh 5300,kitendo kilichopelekea mama huyu kumuadhibu vibaya mtoto wake huyo kama anavyoonekana pichani mtoto Deo,”alinishika kichwa na kunibamiza kwa nguvu kwenye kitanda,na kunichapa kwa bakora kichwani na mwilini”aliongea Deo huku machozi yakimlengalenga,akiongea kwa shida.

Tukio hilo la ukatiri lilifanyika tarehe 22/01/2013 usiku, nakulipopambazuka mtoto Deo alijiandaa kwenda shuleni,alipofika shuleni walimu wake walishitushwa na hali  aliyokuwanayo Deo,walimu walikusanyana na kuchukua hatua ya kuomba msaada ffu ukonga ili mama huyo akamatwe,mama huyo alikamatwa na kufikishwa shuleni,baada ya mahojiano na walimu washule ya Amani,alipekwa kituo cha polisi stakishari ukonga na mtoto alipelekwa hospitari ya Amana kwa ghalama za walimu,na mwalimu mmoja alijitolea kukaa na mtoto kwa siku mbili na motto kurudi kwa mama yake.

Kauli ya mama yake anadai  Deo alijigonga kwenye kitanda,kauli ambayo Deo anaipinga,mototo Deo anatamani  akaishi na baba yake ambae anafahamika kwa jina la Laulent mahali anapoishi hapajajulikana,mtoto Deo anadai kuwa mama yake anamwambia kwa baba yake kuna samba na twiga akienda ataliwa,kauli ambayo inamtisha na kumjengea hofu kwa usalama wa maisha yake. 

1 comment: