Jamii imetakiwa kuacha vitendo vya
ukatiri dhidi ya watoto,badala yake wawalee watoto hao katika malezi bora
yatakayowafanya watoto wawe na furaha wakati wote.
Hivi karibuni maeneo ya ukonga
mazizini katika manispaa ya Ilala,kitendo cha kikatiri dhidi ya mtoto Deo
Laulent,mwenye umri wa miaka 7,anaesoma darasa la kwanza katika shule ya msingi
Amani mzambarauni ukonga,yamemkuta makubwa na kumpelekea kujeruhiwa vibaya
usoni na kichwa kama anavyo onekana pichani.
Kitendo hiki kimedaiwa kufanywa na
mama yake mzazi bi Gradi David,mkazi wa mtaa wa mazizini ukonga,alimuazibu
mtoto kwa kosa la kutokwenda kula chakula kwa mama yake mkubwa baada ya kutoka
shule mchana,kwa maelezo ya mtoto huyu,anakiri kuagizwa kwenda kula kwa mama
mkubwa,lakini akajikuta ameenda kucheza kwa rafiki yake aliyemaja kwa jina la
Juma,kwa maelezo yake mtoto Deo,alicheza kwa rafiki yake,alikula chakula cha
mchana na baadae kuoga kwa huyo rafiki yake,ambapo alishinda huko hadi jioni na
kurudi nyumbani kwao.
Aliporudi nyumbani Deo alipewa sh
1000 na bibi yake[mjumbe wa shina] ambae ni mwenyenyumba alipopanga mama
yake,akanunue chips ale,ambapo bibi huyo hufanya hivyo mara kwa mara,ambapo
mama yake Deo anapotoka kwenye kazi yake hulipa pesa hizo,mama yake Deo ni
muhudumu wa bar maeneo ya banana.
Mama yake Deo,alipokuwa anarudi
toka kazini kwake majira ya usiku alipia kwa muuza chips ambapo mtoto wake
alinunua,akaambiwa mtoto wake amekula chips za tsh 5300,kitendo kilichopelekea
mama huyu kumuadhibu vibaya mtoto wake huyo kama anavyoonekana pichani mtoto
Deo,”alinishika kichwa na kunibamiza kwa nguvu kwenye kitanda,na kunichapa kwa
bakora kichwani na mwilini”aliongea Deo huku machozi yakimlengalenga,akiongea
kwa shida.
Tukio hilo la ukatiri lilifanyika
tarehe 22/01/2013 usiku, nakulipopambazuka mtoto Deo alijiandaa kwenda
shuleni,alipofika shuleni walimu wake walishitushwa na hali aliyokuwanayo Deo,walimu walikusanyana na
kuchukua hatua ya kuomba msaada ffu ukonga ili mama huyo akamatwe,mama huyo
alikamatwa na kufikishwa shuleni,baada ya mahojiano na walimu washule ya
Amani,alipekwa kituo cha polisi stakishari ukonga na mtoto alipelekwa hospitari
ya Amana kwa ghalama za walimu,na mwalimu mmoja alijitolea kukaa na mtoto kwa
siku mbili na motto kurudi kwa mama yake.
Kauli ya mama yake anadai Deo alijigonga kwenye kitanda,kauli ambayo
Deo anaipinga,mototo Deo anatamani
akaishi na baba yake ambae anafahamika kwa jina la Laulent mahali
anapoishi hapajajulikana,mtoto Deo anadai kuwa mama yake anamwambia kwa baba
yake kuna samba na twiga akienda ataliwa,kauli ambayo inamtisha na kumjengea
hofu kwa usalama wa maisha yake.